Monday, May 23, 2016

Ujue Ugonjwa wa BAWASIRI na Tiba zake


Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba.
JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI?
  • Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe 
  • ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles 
  • Tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30-50 
AINA ZA BAWASIRI 
Kuna Aina mbili za bawasiri 
(A) BAWASIRI YA NDANI 
  • Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili 
  • Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa 
  • Aina hii imegawanyika katika madaraja manne 

(1)DARAJA LA KWANZA 
Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika 

(2)DARAJA LA PILI 
Hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia 

(3)DARAJA LA TATU 
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenyewe 

(4)DARAJA LA NNE 
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi 

(B)BAWASIRI YA NJE 
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS 

CHANZO CHA TATIZO 
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
  • KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE 
  • KUHARISHA KWA MUDA MREFU 
  • TATIZO LA KUTOPATA CHOO 
  • MATATIZO YA UMRI 
  • KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU 
  • UZITO KUPITA KIASI 
  • MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU 

DALILI ZA BAWASIRI 
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa 
  • kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia 
  • kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa 
  • kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo 
  • kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana 

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI 
Matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia 

Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia 
  • KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA 
  • KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku 
  • EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU 

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI 
  • kupata upungufu wa damu (anemia) 
  • Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo 
  • hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake 
  • kuathirika kisaikolojia 
  • kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na mau

0 comments:

Post a Comment