Monday, February 6, 2017

Zijue faida ya juice ya MIWA


Kuna faida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo
  •  Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuipatia miili yetu nguvu kwa haraka na kukata kiu, na hii inasababishwa na  sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa itakufaa zaidi.
  • Juisi ya miwa ni tamu lakini pia ni nzuri kwa wagonjwa wa  kisukari,  kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic Index". Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Lakini ni  muhimu kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.
  • Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma na manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser"
  • Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.
  •  Juisi ya miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono  na kidney stones.
  • Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi na Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano
  • Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula.
  • Juisi ya miwa husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo.
  • Huisi ya miwa  husaidia  kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa "constipation".
  • Juisi ya miwa husaidia kuzuia meno kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini.
  • Juisi ya miwa husaidia  kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.
  •  Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha ngozi.
  • Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na kuiimarisha uso ,


0 comments:

Post a Comment