Kuna faida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo
- Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuipatia miili yetu nguvu kwa haraka na kukata kiu, na hii inasababishwa na sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa itakufaa zaidi.
- Juisi ya miwa ni tamu lakini pia ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari, kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic Index". Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Lakini ni muhimu kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.